ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 14, 2017

NAIBU WAZIRI AZINDUA MAZOEZI KWA WANANCHI ILEMELA

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anstazia James Wambura (wa pili kutoka kulia) akikimbia mchakamchaka huku akiwa ameambatana na DC, OCD, Mhazina wa   Manispaa ya Ilemela kuboresha afya asubuhi ya leo.
NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO AZINDUA MAZOEZI YA MWILI KWA WAKAZI WA WILAYA YA ILEMELA

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia James Wambura leo tarehe 14.01.2017 ikiwa ni jumamosi ya pili ya mwezi amezindua mpango wa mazoezi kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Ilemela ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amewataka wananchi na wakazi wa Ilemela ambao leo waliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dr. Leonard Masale, kufanya mazoezi ya mwili kama afanyavyo Rais mstaafu wa awamu ya Pili ambaye kwa sasa ana Zaidi ya miaka 90 na amekuwa akifanya mazoezi takribani saa moja kila siku, kwani mazoezi humfanya mtu kuwa mkakamavu na pia kuzifanya seli za mwili kuufanya mwili kutozeeka/kutochoka mapema.

Tukumbuke kuwa MAZOEZI NDIYO AFYA YAKO, NA AFYA YAKO NDIYO MTAJI WAKO, hivyo ukiwa unafanya mazoezi kutakufanya uwe na afya njema itakayokufanya ushiriki kikamilifu katika shughuli zako za kila siku zinazokuingizia kipato na ndiyo maana tunasema afya yako ndiyo mtaji wako.
Ukiugua magonjwa hasa haya ambayo si ya kuambukizwa kama vile Shinikizo la damu (pressure), Kiharusi au kisukari, ni magojwa ambayo yatakufanya kutofanya kazi kwa muda mrefu lakini pia utatumia gharama kubwa kujitibu, hivyo amewataka wananchi wote kwa ujumla kuyafanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Amesema pia, serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa ya kununua madawa na kutibu wananchi wake, fedha ambayo ingeweza kuwekwa katika shughuli nyingine za kimaendeleo endapo wagonjwa wa magonjwa haya yangeweza kuepukika kwa kufanya mazoezi.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Manispaa ya ilemela na wakazi/wananchi wa Wilaya hii, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Leonard Masale, kwanza amemshukuru Naibu Waziri kwa kuzindua mpango wa mazoezi katika wilaya ya Ilemela, na kuwaelekeza watendaji wa Kata washirikiane na waheshimiwa madiwani kuwaongoza na kuwahamisha wananchi walio katika kata zao kushiriki mazoezi hasa kila jumamosi ya pili ya kila mwezi. Lakini pia amehaidi mazoezi ya mwezi ujao yatashirikisha wananchi wengi kwani leo waliojitokeza wengi ni watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, na baada ya mazoezi hayo wananchi wote watakuwa wakifanya mazoezi katika kata zao.

Pamoja nae, kamanda wa polisi wa Wilaya ya Ilemela, Mrakibu wa Polisi, Evodius Kasigwa, amesema wao polisi wamekuwa wakifanya mazoezi haya kila jumamosi ya wiki.

Mazoezi haya yalianzia katika kiwanja cha Furahisha kwa kutembea matembezi ya Kilomita 3 kwa kupitia mtaa wa Ghana, Kitangiri na kisha kurudi katika uwanja wa Furahisha na kufanya mazoezi ya viungo.

Imetolewa na:
Kizito Bahati
Afisa Michezo

Manispaa ya Ilemela.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.