ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 23, 2016

SHULE YA KIBAHA INDEPENDENT (KIPS) YAWEKA MIKAKATI YA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI

Wanafunzi wa darasa la saba katika  shule  ya msingi ya Kibaha Independent (KIPS) wakionyesha uwezo wao wa kuimba na kucheza kwa furaha  katika mahafali ya 11 iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo. (PICHA NA VICTOR MASANGU)

 NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
KATIKA kuunga juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini uongozi wa shule ya msingi ya Kibaha Independent (KIPS) imesema kwamba inatarajia kujenga majengo mengine kwa lengo la kuweza kuanzisha shule ya sekondari ili kuweza kutoa fursa  elimu kulingana na mahitaji ya wanafunzi wanaohitimu shule za msingi.
 
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Yusuph Mfinanga wakati wa mahafali ya 11 ya shule hiyo ambayo  ni ya binafsi ambapo ameahidi kushirikiana bega kwa began a wadau wengine wa maendeleo sambamba ana serikali katikam tutimiza lengo hilo la kujenga shule ya sekondari.
 
Mfinanga alisema kwamba anatambua katika elimu kuna changamoto nyingi ambazo zinahitajika kutatuliwa ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kuwapa elimu bora ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa katika siku zijazo, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.
 
“kumekuwepo na maombi mbali mbali kutoka kwa wazai kuhusina na kuwepo kwa shule ya sekondari katika Wilaya yetu ya Kibaha ambayo itaweza kuwapa fursa wanafunzi wanaomaliza katika shule za msingi kuweza kujiunga  na kidato cha kwanza wakiwa katika maeneo ya karibu ili kuweza kupata elimu bora zaidi hivyo sualla hili lipo katika mipango yetu,”alifafanua Mfinanga
 
 Katika hatua nyingine Mfinaga aliiomba Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa  wanadumisha zaidi miundombinu ya majengo katika shule mbali mbali sambamba na nyumba za walimu ili kuweza kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
 

Kwa upande wake mmoja wa wazazi akizungumza kwa niaba ya wenzake Selina Wilson walimu  wa shule wanapaswa kuwa waangalizi wa watoto shuleni kwa ukaribu zaidi kwa lengo la kuweza kuwafuatilia mienendo yao na kuepusha wimbi la watoto wanaokwenda kinyume na maadili.
 
 Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Herzon Musalale alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa 2002 kwasasa ina wanafunzi 650 ambapo kwasasa wana matarajio ya kuanzisha shule ya sekondari.

 Akizungumza kwa niaba ya Afisa elimu wa Halmashauri ya mji wa kibaha  Ramadhani Lawoga alisema serikali ipo tayari kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbali mbali wa sekta ya elimu ili kuweza kuona ni namna gani wanaweza kusaidia kwa hali na mali katika kusapoti suala zima la elimu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.