ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 8, 2012

FREEMASONS NA CHAMA CHAO WATINGA MWANZA?

Ni bango lililotundikwa eneo la Kilimahewa wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Kuhusu mawasiliano ambayo yameandikwa chini mwishoni mwa karatasi hiyo ni
0655 905 559
0756 520 154
0789 905 559
0222 405 682

Chunguza mjomba utabaini.

Friday, December 7, 2012

KIOTA KINGINE KIKALI NDANI YA JIJI LA MIAMBA

Ni bwawa la kuogelea lililokamilika sasa ndani ya Isamilo Lodge jijini Mwanza.

Ze engo...

Kwaajili ya pozi mara baada ya kucheza na maji.

Ze bustani here at Isamilo Lodge Mwanza.

Mwanga adimu.

Kitu nature...

ZIMEBAKI SIKU 7 KATI YA 14 WALIZOTOA CHADEMA NYAMAGANA NA ILEMELA KUMTAKA WAZIRI MKUU KUMNG'OA MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA.

Mbunge wa wilaya ya Ilemela Highness Kiwia akihutubia wananchi waliofurika jana jioni kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kwaajili ya kuwasilisha pingamizi la kumkataa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe kwa madai aliyoyatoa ya kutolitendea haki jimbo hilo.

Katika kusanyiko hilo CHADEMA walipitisha karatasi kwa wananchi waliofika viwanjani hapo ili wasaini kuunga mkono hoja ya kumkataa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe na hizi ndizo karatasi za majina na sahihi zilizo kusanywa viwanjani hapo.

Mbunge Ezekiel Wenje (CHADEMA) hakuacha vimbwanga vyake vya kurusha madongo kwa diwani wa Kata ya Kitangiri Henry Matata, ambaye sasa ndiye Meya wa Manispaa ya Ilemela (CHADEMA) akisema kuwa "Watu wa Kitangiri hawakumchagua Matata walichagua CHADEMA, sasa kwa kuwa alitokea CHADEMA, Matata akabebwa na upepo wa CHADEMA  naye akajikuta yumo, Lakini watu wa Kitangiri kimsingi hawakumgia kura Matata, waliipigia kura CHADEMA"

Mmoja kati ya wananchi akisaini karatasi kama mkazi wa ilemela viwanjani hapo kuunga mkono hoja ya kumkataa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe kutokana na sera zilizoainishwa jukwaani na wabunge hao.

Mbunge wa Ilemela Highness Kiwia ameanisha maeneo  yaliyopelekea maamuzi hayo ya kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda kumwondoa mkurugenzi huyo wa jiji kuwa ni pamoja na
1. Kuipa nguvu Halmashauri ya jiji la Mwanza kuendelea kusimamia ugawaji wa viwanja vipatavyo 3500 katika Manispaa ya Ilemela.

2. Uhamishaji wa soko la Mwaloni Kirumba kutoka katika ramani ya Ilemela kwenda Nyamagana.

Mbunge huyo amesema kuwa wakati wa kutoa matamko umepitwa na wakati sasa ni wakati wa vitendo hivyo ofisi yake imejipanga kuhakikisha kuwa ugawaji wa viwanja 3,500 vya Ilemela na soko la Mwaloni Kirumba kubaki kuwa mali ya Ilemela kutokana na vielelezo vya mipaka ya nchi na haki stahiki.

Mbunge wa Musoma mjini Bw. Makongoro naye alikuwepo.

Mpododo-Watu na hisisa zao 'bhana'.

Utulivu wa wananchi kusikiliza kinachojiri akili mkichwa kutafakari.

Hapa karatasi zilizosainiwa zikikusanywa na Red Brigade wa CHADEMA Mwanza ndani ya kusanyiko hilo kusaini kuunga mkono hoja iliyotolewa ya kumkataa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe kutokana na sera zilizoainishwa jukwaani na wabunge hao

Mwananchi akitafakari kabla ya kusaini....

Mwalimu Kamanzi (kushoto) akiwa ameketi na diwani wa kata ya Kirumba Mr. Kahungu mara baada ya kukabidhiwa madawati 10 na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (hayupo pichani) kama sehemu ya shukurani kwa watu wa wilaya ya Ilemela kushiriki vyema kuichangia wilaya ya Nyamagana katika harambee ya madawati kwa shule za msingi iliyofanyika mapema mwaka huu. 

Aliyekuwa mwanachama wa CCM Thomas Pesanga Chacha (mwenye shati jeupe) akinyanyua juu kadi yake mpya aliyokabidhiwa na CHADEMA. Kwa mijibu wa maneno yake jukwaani amesema kuwa, amekuwa mwanachama wa CCM tangu mwaka 1980, akishikilia nyadhifa mbalimbali nafasi yake ya mwisho ni Ujumbe Kamati ya Utekelezaji Baraza la Wazazi Mkoa wa Mwanza aliyoitumikia tangu mwaka 2003 - 2008 kabla ya kutemwa kwenye uchaguzi uliofuata akisota benchi kukosa nyadhifa mbalimbali kwa takribani miaka 5 sasa licha ya kikipenda chama hicho na kukitumikia kwa moyo wote na sasa ameamua kuhamia CHADEMA.

MEYA AONGOZA HARAMBEE YA WANAFUNZI MWANZA KUMCHANGIA KIJANA MWENYE TATIZO LA KIBOFU

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikabidhi kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni mchango wake kwa kijana Dickson Wasiwasi ambaye blogu hii hivi karibuni ilitoa taarifa zake za kushindikana kufanyiwa upasuaji hapa nchini, akihitaji kiasi cha shilingi milioni 20 kwaajili ya kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji. Shughuli hii imefanyika jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba ikiandaliwa na kamati ya Bunge la Watoto  jijini Mwanza na kuwashirikisha wanafunzi wa Sekondari toka shule mbalimbali.

Timu B.

Timu A.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akifanya ukaguzi kwa timu A.

Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akifanya ukaguzi kwa timu B.

Timu A na timu B zikipepetana ndani ya dimba la CCM Kirumba katika mchezo wa hisani kunogesha Harambee hiyo waliyoiandaa kumchangia kijana Dickson Wasiwasi, ambaye ametumikia zaidi ya oparesheni tatu kwenye hospitali ya Rufaa Bugando bila mafanikio na sasa ni juhudi kumpeleka nchini India ambako inaaminika kuna wataalamu waliobobea zaidi watakao msaidia.

Sehemu ya wanafunzi waliojitokeza.

Bunge la Watoto jijini Mwanza likipata picha ya pamoja na Mstahiki Meya, Kamishna wa Chama cha ADC Bw. Ituji, baba na kijana Dickson.

Ambapo wito umetolewa kwa Mashirika, Makampuni, Watu binafsi, Vikundi kujitokeza kumchangia kijana huyu ili akapate matibabu, huu ukiwa ni mwanzo tu wa harakati za vijana hawa wenye mapenzi mema wasiopenda kuona kijana mwenzao akitaabika na kunyanyapaliwa.
 DICKSON VEDASTUS WASIWASI ALIZALIWA 7/07/1996 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA, KIBOFU CHA MKOJO KIKIWA NJE (KIKIONEKANA WAZIWAZI), MADAKTARI WAMEMFANYIA MATIBABU KUPITIA OPARESHENI MARA TATU BILA MAFANIKIO. ZA MATIBABU NI SHILINGI MILIONI 20, NAYE HANA UWEZO HIVYO AMEOMBA WASAMALIA WEMA KUMSAIDIA KUNUSURU ADHA NA MATESO AYAPATAYO MTOTO WAKE.

 CHANGIA KUPITIA AKAUNTI ZIFUATAZO:-
CRDB     0152457709500
AZANIA 003003005102370001

SIMU 0762324527 OR 0683580004

Thursday, December 6, 2012

KUANZA KWA SAFARI ZA TRENI HIYO KESHO UNAFUU KWA WANANCHI NA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA

Wakati kesho (TEREHE 7/12/2012) Treni ya abiria inataraji kuanza upya safari yake kutoka jijini Dar es salaam hadi jijini Mwanza ikiwa ni kutekeleza kwa ahadi ya serikali kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi  Dr. Harson Mwakyembe aliyoitoa Bungeni wakati wa kupitishwa bajeti ya wizara yake.
 Jijini mwanza blogu hii imeshuhudia mafundi pamoja na vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi sehemu mbalimbali ikiwemo zile za kupumzikia abiria  huku pia abiria wakiendelea kukata tiketi zao kwa ajili ya safari ya kwanza tangu kusitishwa takribani miaka mitano siku ya jumapili.


 Kuanza kwa usafiri huo kumerejesha matumaini kwa wananchi wanaotumia usafiri huo hasa kwa wafanyabiashara wanaosafiri na kusafirisha bidhaa kwa wingi kila kukicha kutokana na gharama zake kuwa nafuu zaidi ikilinganishwa na ile ya mabasi ya abiria ya kutoka Mwanza hadi jijini Dar es salaam. 

Bofya Play kusikiliza..


 Hata hivyo changamoto imejitokeza kwa abiria watakao tumia usafiri huo wa treni kwani sasa watalazimika kuwa na vitambulisho au hati za kusafiria, kitambulisho cha mpiga kura au barua ya mwenyekiti wa mtaa anapotoka abiria huyo ili kusaidia kuweka kumbukumbu sahihi kwa abiria waliosafiri kwa siku husika kutambulika pindi  ajali au tatizo lolote linapotokea.
 Njia za treni na mafundi wake.


Mafundi.

Vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi.

Vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi.


Mafundi wapaka rangi wakilikarabati eneo la kuketi abiria  katika maandalizi ya mwisho. 



Nao wadau wa usafirishaji barabarani kwa pikipiki maarufu kama bodaboda nao tayari wameanza kujongea eneo hili ambalo si muda mrefu litarejea kwenye shamrashamra zake kama siku za nyuma ilikuwa mishemishe mchana hadi usiku.

'HAPPY BIRTHDAY WAPENDWAzZ'

"Happy birthday my Supa Queen Oliver J. Ryanna.. This is the sms from your husband Albert G. Sengo.
"Happy birthday mdau mkubwa wa Clouds fm Daudi wa Kota, blogu hii inaungana na wote marafiki wanaokutakia mema maishani"
'Halla'

TANZANIA YOUTH ENTREPRENEURSHIP SUMMIT 2012


STAY CONNECTED

Facebook    Twitter    LinkedIn    Pinterest

UZINDUZI WA MBIO ZA UHURU MARATHON

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akiwasili katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam tayari kwa kuendesha hafla hiyo ya Uzinduzi.akizindua rasmi tovuti ya Mbio hizo ya http://www.uhurumarathon.com pamoja nae ni Mkurugenzi wa Intelecture Communication Ltd, Waandaaji wa Mbio hizo, Innocent Meleck.


Msanii Maarufu wa Nyimbo za Mashaili hapa nchini,Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba akionyesha umahiri wake wa Mashairi yake yenye ujumbe mzito wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akimtunza Mjomba Mrisho Mpoto wakati akiimba nyimbo zake za Mashairi yenye Ujumbe Mzito kwa Taifa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam

Muongozaji wa Hafla hiyo usiku huu,alikuwa ni MC Ephrahim Kibonde.

Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akisoma hotuba yake wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) ambazo zitakuwa zikifanyika kila Mwaka.hafla hii imefanyika katika Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi katika Hafla ya Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akisoma hotuba yake aliyoiandaa wakati wa Uzinduzi wa Uhuru Marathon uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam

utepe...
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mbio za Uhuru (Uhuru Marathon) uliofanyika usiku huu katika Ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es Salaam

Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akitoa ufafanuzi wa mdogo wa nembo na kauli mbiu zitakazo tumika kwenye Mbio hizo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.

Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akimuelezea Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara juu ya Tovuti ya mbio hizo ambayo ni http:// www.uhurumarathon.com muda mfupi baada ya kuzinduliwa.

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara akikabidhiwa fulama Maalum yenye jina la Rais Jakaya Kikwete.

Mratimbu wa Mbio hizo za Uhuru Marathon na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Intellectues Communications Ltd,Innocent Melleck akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon),Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mukangara.
Wadau mbali mbali kutoka makampuni tofauti tofauti hapa nchini pia walikuwepo kwenye uzinduzi huo.

Mjomba Band ikifanya vitu vyake.

Kama newsroom vile
Wanahabari.

SistazZ...
Wadau na meza zao tukioni.

Wadau kibao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.